Kocha Kally Ongara ameungana na mastaa Cleophas Mkandala na Ismail Aziz Kader katika orodha mpya ya mastaa waliotupiwa virago na klabu hiyo ikiwa katika muendelezo wa kujijenga upya kwa ajili ya msimu ujao wa ligi kuu na michuano ya kimataifa.
Kally aliyekua kocha wa timu hiyo lakini kutokana na kutokua na vigezo timu ilikabidhiwa kwa kocha wa makipa Dani Cardena huku Kally akishikilia majukumu yote ya ufundi kwa ujumla japo awali aliajiriwa kama kocha wa washambuliaji.
Pia wachezaji Mkandala na Kader wametemwa kutokana na mapendekezo ya benchi la ufundi chini ya mwalimu mpya wa klabu hiyo Youssouph Dabo ambaye ndie anahusika na masuala ya usajili klabuni hapo kwa sasa.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.