Kaimu Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba SC Ezekiel Kamwaga amekanusha taarifa kuwa ameachishwa kazi na uongozi wa timu hiyo kuhudumu katika nafasi hiyo.
Taarifa hizo zilianza kusambaa jana jioni yakimhusisha kuwa na hali ya sintofahamu kati yake na Mtendaji Mkuu wa timu hiyo Barbara Gonzalenz hali iliyomfanya Ezekiel kutumia ukurasa wake wa Instagram kukanusha.
Ezekiel amesema ”Nimeshangazwa na taarifa hizi zinazosambazwa na waandishi wenzangu wengine waoefu,kuhusu mimi kubwaga manyaga Simba.Nimepewa majukumu yangu mahususi Simba kwa muda wa miezi miwili na bado kazi hiyo sijaikamilisha.Nimedhamiria kukamilisha majukumu hayo hayo mpaka ukomo wake.Mimi bado nipo Simba,tena bado nipo sana.Uongo huu dhidi yangu na Simba SC upuuzwe”. alimaliza