Rais wa shirikisho la soka nchini Wallace Karia amelalamika kuhusu ubora na ufanisi wa waamuzi katika mechi za ligi kuu nchini hususani zile zinazoihusisha Simba sc na Yanga sc kuwa na maamuzi tata yanayoleta maswali na migogoro kwa wadau wa soka nchini.
Karia amesema hayo wakati wa kufunga semina ya waamuzi wa ligi kuu iliyoandaliwa na shirikisho la soka nchini iliyofanyika katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam na kuhuduriwa na idadi kubwa ya waamuzi wa ligi kuu nchini.

