Home Makala Kaze Aomba Wiki Tatu,Yanga Yatoa Maamuzi

Kaze Aomba Wiki Tatu,Yanga Yatoa Maamuzi

by Sports Leo
0 comments

Yanga Sc imetoa maamuzi ya kumbadilisha kocha mpya ambaye ni mrundi,Cedric Kaze aliyetarajiwa kutua bongo siku za karibuni kujiunga na wanasoka hao ili kuwanoa tayari kwa mchuano wa Jumapili wa siku ya wananchi na katika msimu ujao wa ligi kuu bara 2020/2021.

Kaze alikuwa anatarajiwa kuja ndani ya wiki hii kuchukua mikoba ya Luc Eymael raia wa Ubelgiji ambaye alifutwa kazi rasmi Julai 27 kutokana na vitendo vya ubaguzi ila kutokana na kuomba aongezewe wiki tatu mbele,uongozi umeshindwa kumvumilia hivyo kutafuta kocha mwingine.

Uongozi wa Yanga Sc umeshafanya kikao cha dharura leo jioni ili kumpata kocha mwingine kupitia barua ambazo zilitumwa na makocha kuhitaji kazi ndani ya Yanga ili aendelee kunoa kikosi chao kuelekea msimu ujao wa ligi.

banner

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited