Home Makala Kibabage,Kakolanya Wawasili Stars

Kibabage,Kakolanya Wawasili Stars

by Sports Leo
0 comments

Mlinda lango wa klab ya Singida Fountain Gate  Beno David Kakolanya na beki wa kushoto wa klabu ya Yanga sc Nickson Kibabage wamewasili katika kambi ya timu ya Taifa ya Tanzania iliyopo nchini Tunisia kujiandaa na mchezo wa mwisho wa timu hiyo  dhidi ya timu ya Taifa ya Algeria.

Kibabage yeye ameongezwa kwenye Kikosi cha Stars na kocha mkuu Adel Amrouche huku kakolanya aliitwa muda mrefu ila alibakia kumalizia majukumu ya klabu yake ya Singida Fountain Gate  dhidi ya Tabora United uliomalizika kwa suluhu.

Stars ina kibarua kigumu katika mchezo huo ikihitaji alama moja pekee ili ifuzu michuano ya mataifa ya Afrika kwa mara ya tatu katika historia ya nchi.

banner

Kocha Adel Amrouche tayari ana deni kwa watanzani ikizingatiwa wengi wamekua wakishangazwa na uteuzi wake wa kikosi akiwaacha mastaa kama Shomari Kapombe na Mohamed Hussein wa Simba sc.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited