Mshambuliaji wa klabu ya Mbeya City Kibu Dennis ameiongoza timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) katika ushindi wa mabao 2-0 katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa uliofanyika katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.
Mshambuliaji huyo mwenye nguvu akichangia upatikanaji wa mabao mawili ya Taifa stars ambapo bao la kwanza alifanikiwa kumnyang’anya mpira beki wa Malawi kisha kumpasia John Bocco aliyefunga bao la kwanza dakika ya 67.
Kibu pia alisababisha bao la pili kwa Taifa Stars baada ya kuangushwa ambapo mwamuzi aliamuru faulo ipigwe kwenda lango la Malawi ambpo mpigaji Israel Mwenda alifunga bao la pili kwa faulo ya moja kwa moja dakika ya 75.
Mabao hayo mawili yalidumu mpaka mwisho wa mchezo na kuipa alama Stars ambazo zitasaidia kujikwamua katika msimamo wa timu bora huko Fifa.