61
Taarifa kutoka Afrika ya Kusini zinadai tayari Mkurugenzi wa uwekezaji wa GSM na makamu mwenyekiti wa kamati ya mashindano ya klabu ya Yanga, Eng Hersi Said amekubaliana na viongozi wa klabu ya Kaizer Chiefs kumsajili mshambuliaji wa kimataifa wa Zambia Lazarous Kambole kwa mkopo wa mwaka mmoja.
Kambole mwenye umri wa miaka 27 ameshindwa kupata namba kwenye kikosi cha kwanza cha Kaizer Chiefs mbele ya mshambuliaji Samir Nurkovic. Nyota huyo tangu ajiunge na klabu hiyo mwaka 2019 akitokea Zesco United ya Zambia amecheza mechi 14 na kufunga goli moja tu.
Habari hizo zinasema kinachofanyika sasa ni maelewano baina ya mchezaji na klabu ya Yanga sc kuhusu maslahi binafsi ambapo wakikubaliana basi mchezaji huyo atatua kwa mkopo huku kukiwa na kipengele cha kumnunua kabisa.