Kocha wa klabu ya Manchester United Olle Gunnar Solskjaer amewavaa wachezaji wa klabu hiyo baada ya kuruhusu kipigo cha mabao 3-1 kutoka kwa wapinzani wao Manchester city katika mchezo wa kombe la F.A hatua ya nne.
United iliruhusu mabao matatu kipindi cha kwanza yakifungwa na Bernardo Silva dakika ya 17, Riyad Mahrez dakika 33 na Andreas Pereira alijifunga dakika ya 38.
Licha ya Marcus Rashford kufunga bao dakika ya 70 bado haikutosha kutuliza hasira ya kocha huyo kwa wachezaji wake hasa baada ya kuwa nyumbani Old Trafford.