Mshambuliaji wa wakidachi ,Memphis Depay ameripotiwa anaweza kuhama Olympique Lyon baada ya timu hiyo kushindwa kufuzu michuano ya Ulaya kutokana na msimu wa Ligue 1 kusitishwa na bingwa kutangazwa PSG .
Lyon iliyokuwa nafasi ya 7 imeshindwa kupata tiketi ya kucheza michuano ya Ulaya kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 23 baada ya ligi hiyo kuhitimishwa mapema kutokana na janga la Covid-19 na sasa wametishia kwenda mahakamani.
Hata hivyo mmiliki wa klabu hiyo, Jean-Michel Aulas tayari ameibua wasiwasi wake huenda wakapoteza wachezaji wao mastaa akiwamo Depay kama hawatawapa nafasi ya kucheza soka la Ulaya .