David Mapigano Kissu ametambulishwa rasmi kuwa mali ya Azam Fc baada ya kusaini kandarasi ya miaka miwili akitokea klabu ya Gor Mahia ya Kenya.
Kissu alichezea timu za Njombe Mji na Singida United kabla ya kutimkia nchini Kenya pia alikuwa sehemu ya kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars kabla ya janga la virusi vya Corona halijasimamisha masuala ya michezo.
Akiwa na Gor Mahia amecheza jumla ya mechi 15 huku akiwa hajaruhusu nyavu zake kuguswa (clean sheet) katika mechi tisa kati ya hizo na timu yake ilitangazwa kuwa mabingwa wa ligi ya Kenya.