Home Makala Kiungo Stars Anukia Epl

Kiungo Stars Anukia Epl

by Sports Leo
0 comments

Kiungo Novatus Dismas anyeichezea klabu ya Zulte Waregem ambayo imeshuka daraja kutoka ligi kuu ya soka nchini Ubelgiji amezivutia klabu za Southampton na Middlesbrough za nchini Uingereza ambazo zinapambana kuwania saini yake.

Ofa hizo za kumhitaji mchezaji huyo mwenye uwezo wa kucheza kiungo na beki zote za nyuma zimewasili wakati muafaka ambao klabu yake imeshuka daraja hivyo itauza mastaa wengi wa kikosi cha kwanza hasa wenye kiu ya mafanikio.

Novatus amekua akipata nafasi mara kwa mara tangu alipojiunga na timu hiyo msimu uliopita wa kiangazi akitokea Israel ambako alikuwa akiichezea Maccabi Tel Aviv.

banner

Ripoti mbalimbali, Southampton inayoshiriki Ligi Kuu England (EPL) ndio klabu inayoongoza vita hiyo huku wakifuatiwa kwa karibu na Middlesbrough ya Daraja la Kwanza ‘EFL Championship’  na wapo tayari kutoa  Euro 550k (Sh 1.3bilioni).

Taarifa kutoka Ubelgiji, zinasema Zulte Waregem wanaweza kumwachia Novatus na winga wa Gambia Alieu Fadera ambaye anahusishwa na Manchester United katika dirisha hili la usajili ili kupata fedha ambazo zitawafanya kukiboresha kikosi chao kwa ajili ya kuanza maisha mapya ya Ligi Daraja la Kwanza Ubelgiji.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited