Klabu ya Manispaa ya Kinondoni (Kmc) imeibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Namungo Fc katika mchezo wa ligi kuu nchini uliofanyika katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.
Usajili wa Matheo Anthony uliofanyika katika dirisha dogo lililofungwa januari 15 umewalipa Kmc baada ya mshambuliaji huyo kufunga bao la kwanza dakika ya tisa huku pia wakifaidika na usajili wa Charles Ilanfya kwa mkopo kutoka Simba sc aliyefunga pia katika mchezo huo.