Home Makala Kocha Simba Apata Shavu Afrika Kusini

Kocha Simba Apata Shavu Afrika Kusini

by Sports Leo
0 comments

Aliyekuwa kocha mkuu wa Simba Sc kwa msimu wa 2019/2020,Patrick Aussems amepata dili la kuinoa Black Leopard ya Afrika Kusini kwa kipindi cha miaka mitatu.

Aussems raia wa Ubelgiji akiwa ndani ya Simba alifanikiwa kutwaa taji la ligi kuu bara msimu wa 2018/2019 na kukiongoza kikosi hicho kutinga hatua ya robo fainali ya ligi ya mabingwa Afrika.

Simba ilimfungashia virago kocha huyo kutokana na kile kilichoelezwa kuwa alishindwa kusimamia nidhamu ndani ya kikosi hicho.

banner

Patrick anatarajia kuwasili nchini Afrika Kusini wiki ijayo kwa ajili ya kuanza kazi ya kukinoa kikosi hicho ambacho kwa msimu wa 2019/20 ilimaliza ligi kuu ya Afrika Kusini ikiwa nafasi ya 15 na pointi zake 29 baada ya kucheza mechi 30.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited