Kocha wa Barcelona Ronald Koeman amesema kuwa “ana imani lakini hana uhakika” kama mshambuliaji wa Argentina, 33, Lionel Messi atasalia kwenye klabu hiyo msimu huu. (Athletic – subscription required)
Mkataba wa Messi wa pauni milioni 492 na Barcelona ambao unakamilika mwisho wa msimu, unajumuisha kipengee ambacho kinamruhusu kuondoka bila masharti yoyote ikiwa Catalonia itapata uhuru wake. (El Mundo, via Mail)
Mshambuliaji wa Brazil Neymar, 28, atasaini mkataba mpya wa miaka minne na mabingwa wa Ufaransa Paris St-Germain. (Goal)
PSG imetia nia kumuunganisha Neymar na aliyekuwa mchezaji mwenzake Barcelona Messi, katika uwanja wa Parc des Princes. (Metro)
Hatahivyo, mshambuliaji wa Ufaransa, 22, Kylian Mbappe, ambaye mkataba wake na PSG una kamilika 2022, bado hajafanya maamuzi ya hatma yake. (ESPN)
Manchester United huenda imetamatisha nia yake ya kumpata mshambuliaji wa Borussia Dortmund kutoka England Jadon Sancho, 20, baada ya kuvutiwa na winga wa Ivory Coast Amad Diallo tangu alipowasili kutoka Atalanta. Mshambuliaji wa Dortmund raia wa Norway Erling Braut Haaland, 20, na mlinzi wa Sevilla raia wa Ufaransa Jules Kounde, 22, sasa ndio wanaowapa kipaumbele. (Express)
Ombi la Arsenal la kutaka kumsajili mlinzi Junior Firpo raia wa Uhispania, 24, lilikataliwa na Barcelona. (RAC1, via Metro)
Mwenyekiti wa Tottenham Daniel Levy amezuia juhudi za PSG za kumsajili kiungo wa kati wa England Dele Alli, 24, kwasababu ya jeraha lake ambalo linafanya hali yake kuzidi kuwa mbaya. (Telegraph)
Arsenal, Chelsea na Manchester City zote zinamnyatia beki wa kulia wa Inter Milan, 22, raia wa Morocco Achraf Hakimi msimu huu. (Calciomercato – in Italian)
Mshambuliaji kijana raia Jamhuri ya Ireland Sinclair Armstrong, 17, ambaye amehusishwa na Manchester City, Celtic na Crystal Palace, anatarajiwa kuweka saini mkataba mpya na Queens Park Rangers. (TalkSport)
Real Madrid itakuwa tayari kumuuza mshambuliaji wa Brazil, 20, Vinicius Junior msimu huu. (AS – in Spanish)