Home Makala Ligi Kuu Ufaransa Yafutwa

Ligi Kuu Ufaransa Yafutwa

by Sports Leo
0 comments

Serikali ya Ufaransa imezuia kuendelea kwa michezo hadi Septemba mwaka huu, huku Waziri Mkuu wa Ufaransa, Edouard Philippe akisema msimu wa 2019/20 umekwisha kwani hawawezi kuingia uwanjani bila ya mashabiki .

Awali matumaini ya chama cha soka Ufaransa ilikuwa ni kwamba ligi zao zitaendelea Juni 17 na msimu kumalizika Julai 25 baada ya ligi kusitishwa Machi 13 mwaka huu kutokana na kukumbwa na virusi vya corona vilivyoingia Duniani.

Mabingwa watetezi wa Ligue 1, Paris St-Germain wanaongoza ligi kwa tofauti ya pointi 12 mbele ya Marseille, huku Toulouse wapo mkiani wakiwa na pointi 17 juu yao wapo Amiens waliowaacha kwa pointi kumi.

banner

 

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited