Shirikisho la Soka Zanzibar (ZFF) limebainisha kuwa endapo hali itaruhusu na serikali kuruhusu kuendelea kwa michezo visiwani humo, basi ligi hiyo itaendelea kama kawaida baada ya kusimamishwa kwa muda kufuatia mlipuko wa virusi vya Corona visiwani humo .
Serikali ilisimamisha shughuli zote za kimichezo nchini kote ili kupambana na virusi vya Corona vilivyoikumba Dunia, lakini hivi karibuni Rais John Pombe Magufuli aligusia nia yake ya kuruhusu ligi iendelee wakati akimuapisha Mwigulu Nchemba kuwa Waziri wa Katiba na Sheria .
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.