Deogratius Munishl ‘Dida’ambae alikuwa mlinda mlango na mchezaji wa zamani wa vilabu vya Simba na Yanga amekuwa miongoni mwa wachezaji tisa waliosajiliwa kwenye msimu huu wa usajili wa dirisha dogo ndani ya Lipuli Fc.
Simba Sc ilimtema ‘Dida’ mwanzoni mwa msimu huu na hivyo Lipuli ikaamua kumsajili kama mchezaji huru kwa lengo la kuimarisha eneo la ulinzi wa lango lao.
Lipuli pia iliwatema wachezaji wanne ikiwa ni Rajabu Mpululo, Derick Karulika, Waziri Tajiri na Shaban Kimaro.