Klabu ya Real Madrid imeshindwa kutamba mbele ya Manchester City baada ya kukubali kipigo cha mabao 4-0 na kutolewa katika michuano ya klabu bingwa barani ulaya kwa jumla ya mabao 5-1.
Awali jijini Madrid katika mchezo wa kwanza timu hizo zilitoka sare ya 1-1 na mchezo wa marudiano jijini Manchester ndipo dhahama ilipowakuta Madrid kwa kukubali kipigo cha mabao 4-0 huku Benardo Silva akigeuka mwiba kwa kufunga mabao mawili dakika za 23 na 37.
Manuel Akanji alifunga bao la tatu kwa City huku Julian Alvarez akijifunga dakika za mwisho za mchezo na kumfanya kocha Carlo Anceloti akiwa hana la kufanya akiawaacha City wakikata tiketi ya fainali ya michuano hiyo mikubwa barani Ulaya,.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.