Klab ya Ihefu Sc kutoka Mbeya imekamilisha usajili wa winga wa Yanga sc Juma Mahadhi kwa mkataba wa mkopo wa nusu Msimu ambapo mkataba huo utaisha mwishoni mwa msimu huu wa ligi kuu inayoendelea.
Mahadhi bado ana mkataba na Yanga sc lakini majeraha ya muda mrefu ndiyo yaliyosababisha kiwango cha nyota huyo aliyesajiliwa kutokea Coastal union miaka minne iliyopita kutokua na uhakika wa namba kikosini.