Omary Kindamba ambaye ni beki wa Ihefa Fc atakuwa nje kwa muda wa wiki tatu hadi nne kutokana na kupata majeraha ya mbavu baada ya kuanguka vibaya alipokuwa akiitetea timu yake dhidi ya Biashara United,Octoba 14 uwanja wa Karume.
Katika mchezo huo Ihefu ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0 na pointi tatu muhimu kwenda kwa Biashara United.
Ihefu katika msimamo wa ligi kuu ipo nafasi ya 17 baada ya kucheza mechi 6 ikiwa na pointi tatu huku ikiwa imejikusanyia jumla ya mabao mawili.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.