Meneja wa klabu ya Yanga sc Hafidh Salehe ametanabaisha hali ya majeraha katika kikosi hicho kuelekea katika mchezo wa ligi kuu duru la pili dhidi ya Mbeya city utakaofanyika jijini Mbeya.
Kwa mujibu wa meneja huyo mkongwe kati ya mameneja waliohudumu klabu hapo kwa muda mrefu mastaa kadhaa waliokua na matatizo mbalimbali ya kiafya wameanza kurejea katika majukumu yao ya kawaida.
“ Kikosi chetu kina majeruhi wanne ambao ni kiungo mshambuliaji wetu Saido Ntibazonkiza , Michael Sarpong na Yacouba Sogne na beki Dickson Job.
“Yacouba na Saido na Job wote bado waanasumbuliwa na majeraha ya nyama za paja, huku Sarpong yeye akiwa ameumia goti”.
” kuhusu kabwili nae anaendelea vizuri na Ila wote wapo chini ya uangalizi wa madaktari, hii ndiyo sababu walikosekana kwenye mchezo wa Jumamosi dhidi ya African Sports,”