Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda ametimiza ahadi aliyoiahidi ya kumzawadia shilingi milioni 10 kipa wa taifa stars Juma Kaseja kufuatia kiwango bora alichokionyesha dhidi ya Burundi na kuihakikishia ushindi kwa taifa stars.
Kaseja aliyeibuka mchezaji bora wa mechi hiyo aliahidwa kiasi hicho cha fedha na makonda kama sehemu ya motisha kwa wachezaji hao wa timu ya taifa na leo fedha hizo amekabidhiwa rasmi mbele ya kocha wa Taifa stars,Katibu mkuu wa Tff na wachezaji kadhaa waliomsindikiza.
Kaseja amemshukuru makonda kwa kujitoa kwake baada ya kutimiza ahadi kwa muda mfupi huku akisisitiza pesa hiyo ni muhimu na itamsaidia katika kupambana na maisha.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.