Hatimaye Manchester United imemalizana na Alexis Sanchez baada ya klabu ya Inter Milan kukubali kumsajili raia huyo wa Chile kwa pauni milioni 13.5 ambapo mkataba wake utakuwa ni wa miaka mitatu akiitumikia timu hiyo hadi mwezi juni 2023.
Makubaliano ya kumsajili winga huyo yatatangazwa rasmi baada ya mchezo wao dhidi ya Getafe wa michuano ya Europa League siku ya Jumatano.
Sanchez aliibukia ndani ya united msimu wa 2018 akitokea klabu ya Arsenal alipelekwa Inter Milan kwa mkopo msimu wa 2019.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.