Home Makala Man Utd Majanga Tupu

Man Utd Majanga Tupu

by Dennis Msotwa
0 comments

Ni aibu baada ya klabu ya Manchester United kupoteza mchezo wa ligi kuu dhidi y Liverpool baada ya kukubali kichapo kikubwa cha kihistoria cha mabao 7-0 katika mchezo uliofanyika katika uwanja wa Anfield jijini Liverpool mbele ya maelfu ya mashabiki nchini humo.

Ilikua ni siku mbaya kazini kwa Man utd ambapo ilianza kuruhusu mabao mawili ndani ya dakika tano ambapo Cody Gakpo dakika ya 43 na Darwin Nunez dakika ya 47 ambapo kuingia kwa mabao hayo kuliwafungua Man united na hatimaye mvua ya mabao iliwaangukia kupitia kwa Gakpo dakika ya 50 huku Mo salah akifunga dakika za 66 na 83 na msumari wa mwisho ulifungwa na Roberto Firmino dakika ya 88.

Kutokana na kufungwa idadi kubwa hiyo ya magoli kocha wa Man united Eric Ten Hag alitoka kichwa chini huku akisema kuwa ni kosa la timu nzima kuruhusu idadi hiyo ya magoli hasa dhidi ya wapinzani wao wa jadi.

banner

Manchester United pamoja na kipigo hicho imesalia katika nafasi ya tatu ya msimamo wa ligi kuu nchini humo huku Liverpool ikiwa katika nafasi ya tano ya msimamo ikiwa na alama 42.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited