Home Makala Man Utd Wapigwa 3-1

Man Utd Wapigwa 3-1

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya Manchester United imekubali kipigo cha mabao 3-1 kutoka kwa Aston Villa katika mchezo wa ligi kuu nchini Uingereza uliofanyika katika uwanja wa Villa Park nchin humo.

Mpaka kufikia dakika ya 11 Villa ilikua ikiongoza 2-0 kwa mabao ya Leon Badley dakika ya 5 ya mchezo na Lucas Digne dakika ya 11 ya mchezo huku beki Jacob Ramsey akijifunga dakika ya 45 na kufanya timu kwenda mapumziko zikiwa 2-1.

Dakika nne za kipindi cha pili kiliwapatia Villa bao la tatu kutoka kwa Jacob Ramsey aliyefunga bao hilo na kusawazisha makosa yake ya kujifunga ambapo licha ya United kumuanzisha staa Cristiano Ronaldo kama mshambuliaji wa kati akisaidiwa na Marcus Rashford bado Man Utd ilishindwa kupambana na kasi ya Aston Villa.

banner

Manchester United ipo katika nafasi ya tano ya msimamo wa ligi kuu nchini humo ikiwa na alama 23 huku Aston Villa yupo nafasi ya 13 ya msimamo na alama 15 katika mechi 14 alizocheza.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited