Home Makala Man Utd Yaikomalia Atletico Madrid

Man Utd Yaikomalia Atletico Madrid

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya Manchester United imefanikiwa kuondoka na alama moja katika mchezo wa klabu bingwa barani ulaya dhidi ya klabu ya Atletico Madrid katika mchezo uliofanyika katika uwanja wa Wanda Metropolitano jijini Madrid.

Mchezo wa raundi ya kwanza ya hatua ya 16 bora ilishuhudiwa dakika ya 7 tu ambapo Joao Felix akiitanguliza Atletico katika uwanja wa nyumbani akifunga kwa kichwa baada ya kuwazidi maarifa mabeki wa Man United wakiongozwa na Harry Maguire.

Wakiongozwa na Cristiano Ronaldo,Man united walijitahidi kutafuta bao lakini iliwalazimu kusubiri mpaka dakika ya 80 ambapo kinda Anthony Elanga alifunga bao la kusawazisha dakika ya 80 akiunganisha pasi ya Bruno Fernandes na kumuacha kipa Jan Oblak akishangaa.

banner

Sasa mechi hiyo itahamia Old Tarfford jijini Manchester kuamua hatima ya nani atavuka na kuingia hatua ya robo fainali ya michuano hiyo.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited