Home Makala Man Utd Yaipiga Tottenham

Man Utd Yaipiga Tottenham

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya Manchester United imeibuka na alama tatu katika mchezo wa ligi kuu nchini Uingereza dhidi ya Tottenham baada ya kuifunga mabaoa 2-0 katika mchezo mzuri na wa kuvutia uliofanyika katika uwanja wa Old Trafford jijini Manchester.

Man United ambayo inafundishwa na kocha Eric Ten Hag ilianza na mshambuliaji Marcus Rashford aliyesaidiwa na Bruno Fernandes,Anthony na Jadon Sancho huku Tottenham ikiwaanzisha Son na Harry Kane katika eneo la ushambuliaji chini ya kocha Antonio Conte.

Uimara wa Kipa Hugo Lloris uliwasaidia Tottenham kumaliza kipindi cha kwanza kikiwa 0-0 licha ya mashambulizi mazito ya Manchester United kuelekea langoni mwa wageni hao ambapo mashuti ya Rashford,Shaw,Casemiro na Fred yalipanguliwa na kipa huyo kipindi cha kwanza huku David De Gea akipata majaribio ya kawaida kabisa.

banner

Fred aliipatia bao la uongozi Man United mapema kipindi cha kwanza dakika ya 47 na dakika ya 69 Bruno Fernandes alifunga bao la pili na kuifanya United ifikishe alama 19 katika michezo 10 wakiwa nyuma kwa alama nane dhidi ya vinara Arsenal wenye alama 27 huku Manchester City wakiwa katika nafasi ya pili na alama 23 na Tottenham wamesalia nafasi ya tatu na alama 23 katika michezo 11 ya ligi kuu.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited