Licha ya kuanza msimu kwa kusuasua klabu ya Manchester United jana ilipanda mpaka nafasi ya pili ya msimamo wa ligi kuu nchini Uingereza Epl baada ya kuifunga Wolves bao 1-0.
United chini ya Solskjaer imekua na mwendo wa kusuasua lakini imekua ikipata matokeo. ambayo yameifanya ifikishe alama 30 dhidi ya 32 za Liverpool huku wote wakiwa wamecheza michezo 15.
Marcus Rashford alihakikisha ushindi kwa Man utd dakika ya mwisho ya nyongeza 90+3 baada ya mpira kumgonga beki na kubadili mwelekeo na kumuacha kipa Rui Patricio hana la kufanya.