Home Makala Man Utd Yapigwa 4-1

Man Utd Yapigwa 4-1

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya Manchester United imefungwa mabao 4-1 na Manchester City katika mchezo wa ligi kuu nchini Uingereza uliofanyika katika uwanja wa Ettihad jijini Manchester.

Mabao mawili ya Kelvin De Bryune dakika ya 5 na 28 yalitosha kuwatanguliza Man City mpaka kipindi cha kwanza mapumziko ambapo matokeo yalikua 2-1 United wakisawazisha kwa bao la Jadon Sancho alilotupia dakika ya 22 ya mchezo.

Winga rai wa Algeria Riyad Mahrez alitupia mawili dk 68 na 90+1 na kufanya mchezo kumalizika kwa mabao 4-1 huku Man City wakitawala sehemu kubwa ya mchezo huo na kuwaacha United hawana la kufanya.

banner

Kocha wa Manchester UnitedRalf Rangnick amesema:”Nadhani tulikuwa bora kipindi cha kwanza lakini tumepoteza mchezo ni wajibu wetu kuweza kujipanga kwa ajili ya mechi zijazo,”.

Sasa Man city imeendelea kukaa kileleni ikiwa na alama 69 huku Man United ikiwa nafasi ya tano ikiwa na alama 47 katika mbio za ubingwa wa ligi kuu nchini Uingereza.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited