Home Makala Manara Alamba Mamilioni

Manara Alamba Mamilioni

by Sports Leo
0 comments

Afisa habari wa klabu ya Simba Haji Manara amepewa kiasi cha shilingi milioni tatu na mkuu wa mkoa wa Dar es salaam kama zawadi kutokana na mchango wake wa kuhamasisha watanzania waupende mchezo wa soka na kuingia uwanjani.

Msemaji huyo mwenye mbwembwe na majivuno amepewa kiasi hicho cha fedha na mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda leo jijini Dar es salaam,Manara licha ya kuwa msemaji wa simba pia ni mmoja ya wasemaji wenye ushawishi na mvuto mbele ya mashabiki wa soka nchini.

Licha ya mchango wake klabuni hapo pia amesaidia kuhamasisha mashabiki kuipenda na kuishangilia timu ya taifa katika mechi mbalimbali za kufuzu michuano ya Afrika(Afcon) hasa mechi ya mwisho dhidi ya Uganda mechi ambayo stars ilifuzu baada ya kuifunga Uganda magoli matatu kwa bila huku Manara akiwa kiungo muhimu katika kamati ya hamasa iliyojumuisha wasanii na waigiza pamoja na watu maarufu nchini.

banner

Manara ni mtoto wa mchezaji wa zamani wa Yanga Sunday Manara licha ya kwamba yeye ni mshabiki wa Simba timu pinzani na ile anayaishabikia baba yake mzazi.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited