Home Makala Manara Atua Yanga SC Kibabe

Manara Atua Yanga SC Kibabe

by Dennis Msotwa
0 comments

Aliyekua msemaji wa klabu ya Simba sc Haji Manara ameendelea kurusha vijembe kwa mabosi wake wa zamani baada ya kuhamia katika klabu ya Yanga sc kama msemaji mpya wa klabu hiyo akiungana na Hassan Bumbuli na Antonio Nugaz.

Haji wakati wa utambulisho wake katika klabu ya Yanga sc alilisisitiza kuwa amejiunga na mabingwa wa kihistoria na mabingwa mara 27 wa ligi kuu huku akisema kuwa Yanga sc ni timu kubwa hapa nchini.

Msemaji huyo ambaye alikua Mc katika tukio la uzinduzi wa jezi za Yanga sc ambapo alitupa kijembe wa waajiri wake wa zamani kuwa timu hiyo imezindua jezi na sio makorokoko akimaanisha kuwa  jezi hiyo haina matangazo mengi ya biashara za kampuni fulani.

banner

Yanga sc imezindua jezi za aina tofautitofauti kwa ajili ya mechi za nyumbani na ugenini huku pia kukiwa na jezi za kusafiria na jezi za mashabiki ambazo tayari zimeanza kuuzwa mtaani na katika maduka ya Gsm nchini.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited