Home Makala Martial Atua Sevilla

Martial Atua Sevilla

by Sports Leo
0 comments

Mshambuliaji wa klabu ya Manchester united anthony Martial amejiunga na klabu ya Sevilla ya nchini Hispania kwa mkopo wa mpaka mwishoni mwa msimu huu katika kipindi cha majira ya joto.

Martial mwenye umri wa miaka 26 amejiunga na Sevilla Fc inayoshiriki ligi kuu nchini Hispania kwa mkopo wa mizei sita mpaka mwishoni mwa msimu huu ambapo katika dili hilo Sevilla watalipa mshahara wa mchezaji huyo kwa kipindi chote cha mkopo huku kukiwa hakuna dau lolote la usajili lililojumuishwa katika dili hilo.

Mshambuliaji huyo anaondoka United siku chache baada ya kuisaidia klabu hiyo kupata ushindi dhidi ya Westham United katika mchezo wa ligi kuu wikiendi iliyopita huku ameamua kujiunga na Sevilla licha ya kuhitajika pia na Barcelona na Juventus huku akiamini hapo atapata nafasi ya kucheza.

banner

Martial ameichezea Man United michezo 269 akifunga mabao 79 tangu ajiunge klabuni hapo kama mchezaji kinda ghalin zaidi akitokea Monaco Fc ya nchini Ufaransa mwaka 2015.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited