Taarifa zinaeleza kuwa huenda mashabiki wa soka nchini Uingereza wanaweza kurejea tena viwanjani hivi karibuni baada ya mashabiki hao kutoa ombi lililopata saini nyingi bungeni hapo na kupangwa kujadiliwa Novemba 9,mwaka huu.
Serikali ya nchini Uingereza ilipiga marufuku mashabiki kuinga viwanjani tangu mwezi Machi ambapo janga la Corona liliikuta Dunia,hivyo endapo ombi la mashabiki hao likifikiwa muafaka bungeni italeta unafuu kwa vilabu vingi ambavyo vinategemea zaidi mapato ya mlangoni.
Ligi nchini humo imekuwa ikiendelea na mpaka sasa ni raundi ya nne,licha ya kuwa hakuna amshaamsha ya uwanjani ya kuwapa motisha wachezaji.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Msimamo wa ligi kuu Uingereza unaongozwa na Everton ambao wana pointi 12 wakiwa wameshinda michezo yote minne.