Mashabiki wa ngumi waliokuwapo ukumbi wa Next Door Masaki wamegomea bondia Twaha Kiduku kurudiana na Dulla Mbabe kabla hajapigana na Hassan Mwakinyo.
Hiyo ni baada ya Dulla Mbabe kuomba pambano la marudiano hii leo baada ya ushindi wake wa KO lakini mashabiki wa Twaha wamesema wanamtaka kwanza Mwakinyo.
Kwa upande wa bondia Hassan Mwakinyo mara kadhaa amekataa kucheza na bondia huyo akisisitiza kuwa sio saizi yake.