Klabu ambayo nyota Mtanzania,Mbwana Samatta anaichezea nchini England,Aston Villa imepoteza matumaini ya kubaki ndani ya Ligi kuu England baada ya kutoka sare ya bao 1-1 na Everton.
Aston Villa walianza kupachika bao dakika ya 72 kupitia Ezri Konsa ila dakika ya 87, Theo Walcott kutoka Everton aliweza kusawazisha na kupelekea Villa ibaki nafasi ya 19 ikiwa na pointi 31 huku Everton ikiwa nafasi ya 11 na pointi 46 zote zikiwa zimecheza mechi 36.
Wachezaji na benchi la ufundi hawakuwa na furaha baada ya mchezo kwa kuwa waliyeyusha matumaini ya kubaki msimu ujao wa 2020/21 ikiwa ni pamoja na kipa Pepe Reina kwani endapo wangeshinda na kusepa na pointi tatu wangejiongezea nafasi ya kubaki ndani ya ligi.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.