Wachezaji Fiston Mayele na Djigui Diarra wamefanikiwa kupata tuzo katika michuano ya kombe shirikisho iliyomalizika siku ya Jumamosi kutokana na kuonyesha viwango vizuri katika michuano hiyo.
Mayele amefanikiwa kuibuka kuwa mfungaji bora wa michuano hiyo akifunga mabao saba akiwazidi mastaa kama Ranga Chivahiro wa Marumo Gallants huku pia Djigui Diarra akiibuka kuwa mchezaji bora wa mchezo wa fainali ambao Yanga sc walishinda kwa 1-0 japo wamekosa ubingwa kwa sheria ya bao la ugenini.
Diarra amefanikiwa kuibuka kuwa Man of the match katika mchezo huo akifanya uokozi wa mashuti kadhaa huku pia akidaka penati iliyowarudisha Yanga sc mchezoni Yanga sc ambao walikua wanahitaji goli moja zaidi ili kupata ubingwa.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Kipa huyo amekua gumzo nchini na Afrika mashariki kutokana na kiwango chake alichokionyesha katika michuano hiyo huku aina yake ya mpira ukiwemo uwezo wake wa kucheza kwa miguu imemfanya kuwa mchezaji wa ndani wa kumi na mbili hivyo kuipa faida Yanga sc katika michezo mingi.