Home Makala Mazembe yaharibu sherehe Simba day

Mazembe yaharibu sherehe Simba day

by Sports Leo
0 comments

Mabingwa wa DR Congo TP Mazembe wamezima furaha za wanachama,wapenzi na mashabiki wa Simba SC baada ya kuifunga kwa goli 1-0 katika mchezo wa kirafiki uliofanyika katika dimba la Benjamin Mkapa.

Goli la Mazembe lilifungwa kunako dakika ya 84 na mshambuliaji Jean Beleke kwa acrobat akimalizia vizuri mpira wa krosi uliowashinda mabeki wa Simba.

Katika mchezo huo Simba walitawala kipindi cha kwanza japo hawakuwa na madhara na kipindi cha pili Mazembe  walirejea mchezoni na kufanya mashambulizi kadhaa hatimaye kufunga goli pekee la mchezo huo.

banner

Katika matukio mengine katika tamasha hilo,Simba walitambulisha kikosi chao cha msimu ujao.

Katika hatua nyingine Simba SC ilisimama kimya kwa dakika moja kabla ya kuanza kwa mchezo huo kumkumbuka aliyekua mjumbe wa bodi ya wakurugenzi wa klabu hiyo Zacharia Hanspoppe aliyefariki hivi karibuni.

Watu mbalimbali maarufu wamehudhuria tamasha hilo akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Temeke Jokate Mwegelo ambaye alivalishwa jezi ya Simba ikiwa sehemu ya utani wa jadi kwani Jokate ni shabiki kindakindaki wa Yanga.

Uwanja wa Mkapa ulijaa mapema huku mashabiki hao wakiamini kuwa timu yao itapata ushindi kutokana na usajili walioufanya lakini Mazembe wameharibu furaha yao kwa ushindi huo licha ya Simba kuchezesha wachezaji wote wa kimataifa iliyowasajili.

Simba sasa inatarajiwa kumenyana na watani wao wa jana Septemba 25 katika mchezo wa ngao ya hisani kuashiria ufunguzi wa msimu mpa wa ligi kuu soka Tanzania Bara.

 

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited