Home Makala Mbappe Aikoa Psg

Mbappe Aikoa Psg

by Sports Leo
0 comments

Ilibidi Psg kusubiri mpaka dakika ya mwisho ya mchezo ili kupata bao la uongozi dhidi ya Real Madrid katika mchezo wa hatua ya 16 bora ya kombe la klabu bingwa barani ulaya uliofanyika katika uwanja wa Parc des Princes jijini Paris.

Real madrid wakiwa chini ya kocha Carlo Ancelot walijitahidi kucheza kwa nidhamu wakiwazuia Kylian Mbappe,Angel di Maria na Lionel Messi waliokua mwiba mkali kwa viungo Casemiro na Toni Kroos huku kipa Courtous akiokoa mara mbili michomo ya Mbappe.

Mbappe aliangushwa na Carvajal na dakika ya 62 na mwamuzi kutoa pigo la penati kwa Psg lakini Lionel Messi alikosa penati hiyo iliyopanguliwa na kipa Thibaus Courtous.

banner

Sasa Real madrid inabidi isubiri mpaka 9 mwezi machi kuweza kulipiza kisasi ili kupata nafasi ya kufuzu robo fainali ya michuano hiyo.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited