Rasmi Klabu ya Mbeya City imekamilisha usajili wa Touya Jean Didier, mshambuliaji kutoka Burundi aliyekua akichezea Musanse FC ya nchini kwao Burundi.
Timu hiyo ipo katika kujiimarisha na tayari imemnasa David Mwasa kutoka Kmc kwa mkopo huku pia imekamilisha usajili wa Yayo Kato Lutimyba, beki wa kushoto kutokea Sports Club Villa ya Uganda. Pia, Yayo ni mchezaji nyota wa Ugandan the Cranes (Timu ya Taifa ya Uganda).