Home Makala Mchezaji Uturuki Akiri Kumuua Mtoto Wake

Mchezaji Uturuki Akiri Kumuua Mtoto Wake

by Dennis Msotwa
0 comments

Beki wa klabu ya Bursa Yildirim Spor, Cevher Tokts ambaye ni raia wa Uturuki amekiri kumuua mtoto wake kwa kuwa alikuwa hampendi na kujisalimisha polisi.

 

Tukio hilo la mauaji lilitokea Aprili 23, mwaka huu ambapo beki huyo alimpeleka mtoto wake huyo wa miaka mitano hospitali baada ya kuonyesha dalili za virusi vya Corona lakini baadaye aliwaambia wauguzi kuwa mtoto wake alikuwa na tatizo la kushindwa kupumua hivyo alipelekwa chumba cha Wagonjwa Mahututi (ICU) na kisha kufariki.

 

Hata hivyo baada ya siku kadhaa mchezaji huyo alijipeleka Polisi mwenyewe na kukiri amemua mtoto wake kwa sababu alikuwa hampendi.

 

banner
Mchezaji huyo alisema: “Mtoto alikuwa amelala nikachukua mto na kuweka kichwani na kumfumba mdomo kwa dakika 15 hii ni kwa sababu nilikuwa simpendi tangu alipozaliwa na sijui kwa nini na ndiyo maana niliamua kumuua sababu nilikuwa simtaki na sina tatizo lolote la akili.”alikiri beki huyo mbele ya polisi.

 

Hata hivyo kwa sasa Polisi wa Uturuki bado wanamshikilia mchezaji huyo na huenda akafungwa kifungo cha maisha.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited