Home Makala Mgunda Atimka Mashujaa Fc

Mgunda Atimka Mashujaa Fc

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya Mashujaa Fc  imefikia makubaliano ya kusitisha mkataba wake na mshambuliaji  Ismail Mgunda  baada ya kufikia makubaliano na klabu ya As Vita ya Congo DRC.

As Vita inayonolewa na kocha wa zamani wa klabu ya Azam Fc Youssouph Dabo ambaye alivutiwa na mshambuliaji huyo na kuanza harakati za kumsajili ambapo walifikia makubaliano binafsi na mchezaji huyo huku ikibaki kumalizana na timu yake.

banner

Mgunda alibakisha mkataba wa mwaka mmoja na nusu na wazee wa mapigo na mwendo sasa ni mali ya AS vita baada ya dili hilo kukamilika kwa klabu hizo kufikia makubaliano.

Mgunda mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Jomo Cosmos ya nchini Afrika ya kusini pamoja na vilabu vya Ruvu Shooting na Singida United Fc ana mwili mkubwa wenye misuli ambayo huwasumbua mabeki wa timu pinzani sambamba na uwezo wake wa kasi pamoja na kufunga.

Kocha Yousouph Dabo ameona kuwa mshambuliaji huyo ataisaidia klabu yake katika ligi kuu ya nchini Dr Congo.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited