Home Makala Minziro Kutua Pamba Jiji

Minziro Kutua Pamba Jiji

by Sports Leo
0 comments

Imefahamika kuwa Kocha Fred Felix Minziro atachukua mikoba ya Goran Kopunovic ambae amefutwa kazi Pamba Jiji Fc kutokana na matokeo yasiyoridhisha katika ligi kuu ya Nbc nchini.

Minziro ataenda Pamba Jiji Fc akiwa na wasaidizi wake akiwemo Mathias Wandiba ambae ameshafanya nae kazi Geita Gold fc na kwa sasa tayari kocha huyo msaidizi yupo na kikosi jijini Mwanza.

Minziro ambaye kwa sasa anainoa timu ya Big Man Fc zamani ikijulikana kama Mwadui Fc akisaidiwa na Uhuru Selemani ambapo amelazimika kuiacha timu hiyo na kuelekea jijini Mwanza kukamilisha usajili wa kujiunga na Pamba Jiji Fc.

banner

Kuajiriwa kwa Minziro klabuni hapo akiwa na wasaidizi wake kunamaanisha kuwa sasa klabu huyo itaachana na waliokua wasaidizi wa Goran ambao ni kiungo wa zamani wa Yanga sc Salvatory Edward na Kocha wa makipa Razack Siwa rai wa Kenya.

Pamba Jiji tangu ipande daraja kuja katika ligi kuu ya Nbc msimu huu mpaka sasa haijaonja ushindi wowote katika michezo saba ya ligi kuu ya Nbc nchini.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited