Klabu ya Simba Sc imekamilisha usajili wa beki wa kushoto wa Coastal Union ya jijini Tanga Miraji Abdallah ‘ZAMBO kwa mkataba wa miaka mitatu kuziba pengo la Mohammed Hussein Zimbwe.
Miraji Zambo ni miongoni mwa wachezaji waliopewa mkataba wa muda mrefu ndani ya Simba Sports Club ili kutoa nafasi ya kukua zaidi wakiamini kuwa anakwenda kuziba nafasi hiyo ambayo imewashinda mabeki wengi kikosini humo.
Simba Sc na Zimbwe Jr wameshindwana katika suala la maslahi binafsi ambapo tayar mchezaji huyo ameshaaga akienda kutafuta changamoto nyingine ambapo mpaka sasa inasemekana kuwa anajiunga na Yanga sc.
Miraji ambaye amekua nahodha wa Coastal Union ameonyesha kiwango bora sana akijitahidi katika eneo la kushoto la klabu hiyo kutimiza majukumu ya kushambulia na kukaba kwa pamoja licha ya kukutana na washambuliaji wazoefu nchini.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Simba sc imeanza kuwapima afya wachezaji wake wa zamani na wapya huku ikiweka wazi kuwa ina mpango wa kuweka kambi nchini Misri ya maandalizi ya msimu wa 2025-2026.