Site icon Sports Leo

Mkude Aondoka Simba sc

Baada ya kudumu katika kikosi cha Simba sc kwa takribani miaka 13 tangu asajiliwe rasmi katika timu ya wakubwa ya klabu hiyo akitokea Simba sc hatimaye kiungo wa klabu hiyo Jonas Mkude rasmi anaondoka klabuni hapo baada ya mkataba wake kuisha.

Simba sc wameafikiana kuachana na mchezaji huyo kutokana na mapendekezo ya benchi la ufundi katika kuboresha timu hiyo ambapo wametaka watafutiwe kiungo mwingine kuongeza nguvu kuungana na Mzamiru Yassin na Sadio Kanoute.

Tayari timu za Singida Fountain Gate Fc imeonyesha nia ya kumchukua staa huyo kuziba nafasi ya Yusuph Kagoma ambaye yupo mbioni kujiunga na Yanga sc.

Mpaka sasa Simba sc tayari imeachana na mastaa kadhaa kama vile Gadiel Michael,Victor Akpan,Mohamed Outtara,Erasto Nyoni,Beno Kakolanya,Nelson Okwa huku pia ikisafisha baadhi ya watu wa benchi la ufundi.

Exit mobile version