Site icon Sports Leo

Mo Afunguka Mambo Mazito Simba Sc

Mo Afunguka Mambo Mazito Simba Sc

Tajiri wa klabu ya Simba sc Mohamed Dewji maarufu kama Mo Afunguka Mambo Mazito Simba Sc kuhusu mstakabli wa klabu hiyo kuelekea msimu ujao wa ligi kuu na michuano ya kimataifa akiahidi kufanya usajili mzito wa mastaa mbalimbali sambamba na kufafanua mambo kadhaa.

Tajiri huyo ambaye anamiliki asilimia 49 ya hisa za klabu hiyo kwa mujibu wa mkataba wa uwekezaji klabuni hapo alifunguka kwa njia ya video akianza kwa kuelekezea namna anavyomwaga fedha kwa ajili ya mambo mbalimbali ya klabu hiyo ikiwemo usajili na kusaidia kulipa mishahara na posho mbalimbali.

“Hadi sasa ndani ya Simba SC nimetumia Bilioni 45 kwa ajili ya mishahara, usajili na gharama za uendeshaji, nimewekeza Bilioni 20 na nimetoa Bilioni 22 fedha ambazo hazipo kwenye mfumo rasmo hivyo nimetoa jumla ya Bilioni 87”,Alisema akifafanua maswali ya mashabiki,wanachama na wadau mbalimbali wanaohoji kuhusu utoaji fedha wa bosi huyo katika klabu hiyo.

Nje na hilo tajiri huyo aliwatoa hofu mashabiki,wanachama na wapenzi wa klabu hiyo kuhusu usajili wa mastaa mbalimbali kwa ajili ya msimu ujao ili kukata ukomo wa mataji klabuni hapo ambapo mpaka sasa imepita miaka minne mpaka sasa hawajachukua kombe la aina yeyote.

“Nimetenga fedha za kutosha kuhakikisha timu yetu inakuwa bora zaidi kwa neena ya mungu Simba itajulikana kwa makubwa zaidi, nimewekeza muda wangu, nimewekeza jasho, damu na fedha katika Simba kwa mapenzi ya dhati kwa klabu hii”,Alimalizia kusema bosi huyo.

Mashabiki wa Simba sc nchini wamekua na maoni mbalimbali kuhusu mambo ya kiuongozi klabuni humo wakilalamikia uongozi wa klabu hiyo kuwa haufanyi usajili wa mastaa wa maana ndio maana mpaka sasa wameshindwa kuchukua mataji wakiwaachia watani zao Yanga sc kuchukua ubingwa waligi kuu kwa mara ya nne mfululizo msimu huu.

Mbali na kuchukua mataji yote misimu takribani mitatu sasa bado pia Simba sc imekubali kipigo kutoka kwa Yanga sc takribani msimu wa nne sasa wamekua wakifungwa ikiwemo kipigo cha fedheha cha mabao 5-1 walichokipa machi 20 2024 katika uwanja wa Benjamini Mkapa.

Hata hivyo pamoja na kujitokeza kwa Mo Dewji kujibu maswali bado baadhi ya wadau wa soka wameanza kuhoji kuhusu fedha hizo anazotoa nje ya mfumo zinakwenda wapi na huwa zinatoka kwa ajili ya masharti gani huku pia wakimataka kutaja faida anazofaidika kama mdhamini wa klabu hiyo pindi matangazo ya bidhaa zake yanapokaa katika jezi za klabu hiyo.

Exit mobile version