Klabu ya Simba sc imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Dodoma Jiji Fc huku Benard Morrison akipeleka mauaji katika mchezo huo uliofanyika katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.
Morrison alipiga krosi iliyounganishwa kwa kichwa na Meddie Kagere na kumshinda kipa Aron Kalambo na kuiandikia Simba sc bao la uongozi lililodumu kwa dakika 6 tu ambapo Cleofas Mkandala alisawazisha bao hilo kwa kichwa dakika ya 36 ambapo mpaka mapumziko mechi ilikua 1-1.
Kipindi cha pili dakika ya 67 pasi ya Perfect Chikwende ilimkuta Benard Morrison aliyepiga shuti kali lililozama wavuni na kuisaidia Simba sc kupata alama tatu katika mchezo huo mkali na wa kusisimua.
Simba sc sasa imefikisha alama 38 katika msimamo ligi kuu huku ikiwa imecheza jumla ya michezo 16 ambapo imebakiza michezo miwili ili kumaliza viporo vya mzunguko wa kwanza.