Home Makala MRI Yashikilia Hatma ya Samatta

MRI Yashikilia Hatma ya Samatta

by Sports Leo
0 comments

Hofu ilikua imetanda katika klabu ya Krc Genk anayoichezea Mtanzania Mbwana Samatta kufuatia kupata jeraha katika goti hali iliyosababisha kupelekwa kwenye mashine ya Magnetic Resonance Imaging.

Jeraha hilo alilipata katika mechi ya Taifa Stars dhidi ya Burundi hali iliyomlazimu kocha Ettiene Ndayiragije kumtoa nahodha huyo na nafasi yake kuchukuliwa na Himid Mao Mkami.

Samatta akiingizwa kwenye mashine ya MRI kujua ukubwa wa jeraha la goti aliloumia.

Licha ya kuonekana na barafu katika goti hilo akiwa katika benchi la timu ya taifa staa huyo alipaa na na ndege kwenda Ubelgiji na aliundiwa jopo la madaktari kumi ambao walimfanyia vipimo hivyo kwenye mashine hiyo inayotumia sumaku na mawimbi ya redio kujua tatizo lililopo.

banner

Habari njema zilizothibitishwa na mchezaji huyo kupitia mtandao wa Instagram ni kwamba vipimo hivyo vimeonesha jeraha hilo sio kubwa hivyo itamlazimu kupumzika kwa siku kadhaa huku akifanya mazoezi mepesi baada ya goti hilo kutikisika kiasi japo endapo angeumia zaidi angekabiliwa na mapumziko ya miezi sita.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited