Home Makala Msuva Anukia Mazembe

Msuva Anukia Mazembe

by Sports Leo
0 comments

Winga Mtanzania Simon Msuva anatajwa kuwa kwenye rada za matajiri wa soka barani Afrika Tp Mazembe yenye maskani yake Lubumbashi nchini Congo ambapo inasemekana tayari uongozi wa timu hiyo upo nchini kufanya mazungumzo na staa huyo msumbufu kwa mabeki kutokana na kasi yake uwanjani.

Inafahamika Msuva ambaye ana mgogoro na klabu yake ya Wydad Casablanca kutokana na klabu hiyo kutompa stahiki zake hali iliyopelekea Msuva kuchukua uamuzi wa kugoma kufanya mazoezi na kupeleka madai yake katika shirikisho la soka duniani(Fifa) ili kupata haki yake.

Hivi sasa mchezaji huyo yupo jijini Dar es salaam akiendelea na mazoezi binafsi huku akisubiri uamuzi wa Fifa kuhusu madai yake lakini pia anaweza kujiunga na klabu nyingine ili asipoteze kiwango chake kwa mujibu wa kanuni za Fifa.

banner

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited