Mshambuliaji chipukizi wa Tanzania Kelvin John ‘Mbappe’ ambaye anaichezea timu ya vijana wenye umri chini ya miaka 20 Ngorongoro Heroes ya Tanzania amejiunga rami na klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji ambayo nahodha wa timu ya taifa Tanzania Mbwana Samatta alikuwa akicheza.
Kelvin John amekuwa mrithi wa nafasi ya Samatta baada ya nahodha huyo kujiunga na Aston Villa inayoshiriki ligi kuu ya Uingereza.
Meneja wa mchezaji huyo Mbaki Muhataba amesema kuwa uongozi wa Genk umevutiwa na uwezo aliokuwa nao kijana huyo na anasubiriwa afikishe miaka 18 mwaka huu pia amalizie masomo yake katika chuo cha Brooke House nchini Uingereza.