Mtanzani Tepsi Evance Theonasy kutoka Cambiasso Sports aliyekuwa akichezea timu ya vijana chini ya umri wa miaka 20 Azam Fc na Ngorongoro Heroes amewasili Ufaransa katika klabu ya FC Nantes kwa ajili ya kukuzwa kisoka hadi atakapotimiza miaka 18 mwaka huu.
Tepsi alichukuliwa katika Clinic ya Cambiasso Sports na Rainbow Sports mwishoni Novemba 2019 uwanja wa Uhuru akiwa chini ya scout maarufu kutoka Rainbow Sport ,Alex Morfaw.
Baada ya mchezaji huyo kutimiza miaka 18 atasajiliwa rasmi na timu ya wakubwa Fc Nantes ambayo ni miongoni mwa klabu zinazoshiriki ligi kuu nchini Ufaransa.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.